1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Mapambano ya risasi yaendelea huko Islamabad

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBm0

Mapambano ya risasi yamezuka tena leo hii katika msikiti uliotekwa mjini Islamabad siku moja baada ya mapambano yaliyosababisha kuuwawa kwa watu 16. Wanafunzi kwenye msikiti huo walifyatuliana risasi na vikosi vya usalama baada ya polisi kurusha gesi ya kutoa machozi katika msikiti huo. Viongozi wenye itikadi kali wa msikiti wa Lal Masjid mjini Islamabad wamekataa kusalimu amri baada ya kumalizika muda uliowekwa na serikali wa kuwataka wajisalimishe.

Zaidi ya wafuasi wao 700 wamejisalimisha wakati vikosi vya wanajeshi wa serikali vikiimarisha usalama nje ya msikiti huo.

Takriban watu kumi waliuwawa hapo jana katika mapambano ya risasi kati vikosi vya polisi na wanafuanzi wenye itikadi kali.

Wapatanishi wa mzozo huo ambao ni wanadini wameshindwa katika majaribio ya kutafuta suluhu .

Wanafunzi wenye msimamo mkali wa kidini wanaowaunga mkono viongozi wao wa kidini wanataka kuanzisha sheria ya kiislamu inayofuata mfumo wa kitaliban katika mji huo wa Islamabad.