1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD.Makamu wa rais wa Marekani yuko nchini Pakistan

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOH

Makamu wa rais wa Marekani Dick Cheney amefanya ziara ya ghafla nchini Pakistan kufanya mazungumzo na rais Parves Musharaf.

Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kutathmini mashambulio yanayopangwa na wanamgambo wa Taliban baada msimu huu wa baridi kumalizika katika nchi jirani ya Afghanistan.

Bwana Cheney amekutana na rais Parves Musharaf katika mji wa Islamabad na wamezungumzia juu ya mikakati ya ushirika.

Habari zaidi zinasema kuwa waziri wa mambo ya nje wa Uingereza bibi Margaret Beckett pia alizunguzma na rais Musharaf juu ya swala la Taliban.