1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Maelfu waandamana kumuunga mkono jaji

6 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4Y

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika barabarani, mjini Islamabad, katika kumuunga mkono Jaji Mkuu wa nchi hiyo Iftikhar Chaundhry aliyesimamishwa kazi.

Jaji Mkuu huyo alikuwa njiani kuelekea katika mji wa Lahore, ambako atahutubia kutafuta uungwaji mkono katika mapambano yake dhidi ya jaribio la Rais Pervez Musharraf la kumfukuza kazi.

Rais Musharraf alimsimamisha kazi Jaji Mkuu huyo mwezi Marchi kwa tuhuma za kutumia vibaya madaraka, hatua ambayo ineonakana na wananchi pamoja na upande wa upinzani kama kupiga vita uhuru wa mahakama.