1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD:Hatimaye Musharraf kwenda Afghanistan

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaG

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan anatarajiwa kuelekea Kabul Afghanistan mwishoni mwa wiki kuhutubia mkutano wa wakuu wa makabila ya Pakistan na Afghanistan wanaokutana nchini humu kuzungumzia mikakati ya kupambana na wanamgambo wa Kitaleban na Al Qaida.

Wizara ya Mambo ya nje ya Pakistan imesema kuwa Rais Musharraf amekubalia kuhudhuria kipindi cha mwisho cha mkutano huo wa siku nne baada ya hapo jana kuombwa hivyo na Rais Hamid Karzai wa Afghanistan.

Mapema Musharraf aliahirisha kwenda katika mkutano huo kutokana na kile alichosema kushughulikia matatizo ya ndani.Kutokuwepo kwake kumeuathiri kwa kiasi fulani mkutano huo uitwayo Jirga ambapo zaidi ya wajumbe 650 wanahudhuria.