ISLAMABAD:Hakuna sheria inayomzuia Musharraf kubakia na cheo | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD:Hakuna sheria inayomzuia Musharraf kubakia na cheo

Rais Pervez Musharraf imeelezwa kuwa ana nia ya kubakia na cheo cha ukuu wa majeshi iwapo atashindwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwezi ujayo.

Mwanasheria Mkuu wa Pakistan Malik Mohamed Qayyum ameiambia mahakama kuu ya nchi hiyo kwamba hakuna kikwazo cha kisheria kinachomzuia Generali Musharraf kuendelea na wadhifa huo.

Upande wa upinzani ulifungua kesi katika mahakama hiyo ukipinga uhalali wa Musharraf kugombea urais wakati akiwa na cheo cha ukuu wa majeshi.

Mahakama hiyo inatarajiwa kutoa uamuzi juu ya kesi hiyo katika siku chache zijazo.Generali Musharraf mwenyewe ameahidi kung´atuka katika nafasi ya ukuu wa majeshi iwapo atashinda katika uchaguzi huo wa tarehe 6 mwezi ujayo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com