1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Watu takriban 13 wanyongwa

Watu takriban 13, wakiwemo maafisa sita wa usalama wa Pakistan wamenyongwa na wanamgambo walio wafuasi wa kundi la Taliban katika eneo la kaskazini la Pakistan linalokabiliwa na machafuko.

Mauaji hayo yamefanyika baada ya mapambano makali kati ya vikosi vya usalama na wanamgambo wa kiislamu wenye siasa kali ya kidini kwenye bonde la Swat katika jimbo la kaskazini magharibi.

Duru za polisi zinasema maafisa sita wa polisi na wanajeshi waliopatikana walikuwa wamekatwa vichwa.

Mashambulizi ya wanamgambo yamekuwa yakiongezeka katika bonde la Swat tangu shehe anayeliunga mkono kundi la Taliban, Maulana Fazlullah, alipowatolea mwito watu wajiunge na vita vya jihad dhidi ya serikali ya Pakistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com