ISLAMABAD: Watu 13 wauawa Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 31.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Watu 13 wauawa Pakistan

Watu waliokuwa na bunduki wameivamia nyumba ya afisa mmoja mkuu wa serikali na wakawaua watu kumi na watatu katika eneo la kaskazini mashariki mwa Pakistan.

Mauaji hayo yalitekelezwa karibu na mji wa Tank katika mkoa wa Kaskazini Mashariki.

Mji wa Tank ndicho kituo cha kuingia kwenye eneo la Waziristan Kusini karibu na mpaka wa Afghanistan, eneo ambalo kuna waungaji mkono wengi wa kundi la al-Qaeda pamoja na wanamgambo wa Taliban.

Eneo hilo limekuwa lilikabiliwa mashambulio makali juma lililopita.

Polisi wa Waziristan Kusini wanachunguza sababu za shambulio hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com