1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Watakiwa kutoka msikitini ama sivyo watauwawa.

8 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkw

Rais wa Pakistan Jenerali Pervez Musharaff ameondoa uwezekano wowote wa kupatikana muafaka na Waislamu wenye msimamo mkali waliojificha ndani ya msikiti mjini Islamabad kwa karibu wiki moja sasa.

Musharraf anaripotiwa kuwa amewaambia viongozi wa msikiti huo kuwaachilia mara moja wanawake na watoto , la sivyo watauwawa.

Wanajeshi na magari ya jeshi yenye silaha yameuzingira Msikiti huo , ambako mamia ya watu wamejifungia ndani tangu Jumanne iliyopita, wakati wanafunzi wanaharakati waliposhambulia kituo cha polisi cha upekuzi.

Kiongozi wa kidini mwenye msimamo mkali anayeoongoza upinzani huo amesema kuwa yeye pamoja na wafuasi wake wana chakula cha kutosha pamoja na silaha ndani ya eneo la msikiti huo ambapo wanaweza kuishi kwa muda wa zaidi ya mwezi.