1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Vikosi vya serikali vyapambana na wanamgambo

2 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Aj

Nchini Pakistan,mapigano yanaendelea kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wanaowaunga mkono Wataliban.Ripoti zinasema,hadi wanamgambo 70 wameuawa katika mapigano hayo kaskazini-magharibi ya nchi.Katika shambulizi jingine katika mji wa Sarghoda,katikati ya Pakistan, mwanamgambo aliejitolea maisha muhanga,ameua si chini ya watu 8.

Machafuko haya yanatokea wakati Mahakama Kuu ikingojewa kutoa uamuzi wake,iwapo hatua iliyochukuliwa hivi karibuni kumteua Rais wa Pakistan,Pervez Musharraf kugombea tena uchaguzi wa rais inaruhusiwa kikatiba.

Kuna hofu kuwa Rais Musharraf huenda akatangaza hali ya hatari,ikiwa Mahakama Kuu itapinga hatua iliyochukuliwa.Mahakama Kuu imesema,uvumi huo hautoshawishi uamuzi wake.