1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Rais wa zamani wa Pakistan afariki dunia

Rais wa zamani wa Pakistan, Ghulam Ishaq Khan, ameaga dunia leo akiwa na umri wa miaka 91 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Waziri wa utawala wa mikoa wa Pakistan, Salim Saifullah, amesema kiongozi huyo wa zamani amefariki dunia leo asubuhi.

Khan alizaliwa mwaka wa 1951 na aliwahi kuwa waziri wa fedha wa Pakistan kabla kuwa rais mwaka wa 1988 kufuatia kifo cha kiongozi wa kijeshi, Jenerali Zias ul Haq kwenye ajali ya ndege.

Khan alifutilaa mbali serikali ya Benazir Bhutto mwaka wa 1990 na serikali ya Nawaz Sharif mnamo mwaka wa 1993, kwa ufisadi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com