1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD: Rais wa Uchina, Hu Jintao aitembelea Pakistan

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCpr

Rais wa Uchina, Hu Jintao, amewasili nchini Pakistan kwa mazungumzo yanayolenga kuinua uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili. Ziara hiyo nchini Pakistan imefuatia ziara ya siku 4 aliyoifanya nchini India ambako alikubaliana na waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, kuongeza mara mbili kiwango cha biashara na kufikia dolla bilioni 40 hadi kufikia mwaka 2010. Akiwa nchini Pakistan, Hu Jintao na mwenzie Pervez Musharraf, wanatarajiwa kusaini mktaba wa biashara huru, kwa lengo la kuongeza mara tatu biashara manmo muda wa miaka mitano ijayo.

Ziara ya Hu Jintao nchini Pakistan ndio ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Uchina kwa muda wa miaka 10 iliopita.