ISLAMABAD: Rais Musharraf ameahidi kuacha madaraka ya kijeshi | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Rais Musharraf ameahidi kuacha madaraka ya kijeshi

Rais wa kijeshi wa Pakistan,Jemadari Pervez Musharraf ametetea uamuzi wake wa kutangaza hali ya hatari.Alipozungumza na waandishi wa habari mjini Islamabad,Musharraf vile vile aliahidi kujiuzulu jeshini na kuapishwa kama rais pale Mahakama Kuu itakapoidhinisha hatua iliyomchagua kuendelea na wadhifa huo.Kiongozi huyo wa kijeshi akaongezea,uchaguzi mkuu unapaswa kufanywa kabla ya tarehe 9 Januari lakini hakutaja tarehe ya kuondosha hali ya hatari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com