1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Musharaff awasilisha fomu za kuwania urais

27 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMC

Waziri Mkuu wa Pakistan amewasilisha nyaraka zenye kumteuwa Rais Pervez Musharraf kuwania uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika nchini humo tarehe 6 mwezi wa Oktoba.

Shaukat Aziz na viongozi wengine waandamizi wa serikali wamewasilisha nyaraka hizo katika Tume ya Uchaguzi mjini Islamabad.Mamia ya polisi wa kutuliza ghasia na makamandoo wamewekwa karibu na jengo la tume hiyo na barabara zote kuelekea kwenye ofisi hiyo zimefungwa na vikosi vya usalama.

Serikali imewatia mbaroni mamia ya wafanyakazi wa upinzani na viongozi katika misako iliokusudia kuvunja upinzani dhidi ya mpango wa Musharraf kuwania kipindi cha pili madarakani.