Islamabad. Makombora yaelekezwa katika jengo la bunge. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Islamabad. Makombora yaelekezwa katika jengo la bunge.

Wataalamu wa kutegua mabomu wametegua makombora mawili ambayo yalikuwa yameelekezwa katika jengo la bunge la Pakistan.

Makombora hayo, ambayo yalikuwa yamefungiwa simu za mkononi, yaligunduliwa karibu na vichaka kiasi cha mita 750 karibu na jengo la bunge la taifa leo asubuhi.

Rais Pervez Musharaff alikuwa akihutubia mkutano wa waandishi wa habari kiasi cha kilometa mbili kutoka katika eneo hilo.

Katika tukio tofauti, maafisa wanachunguza mlipuko mkubwa uliotokea karibu na nyumba ya rais Musharaff jana jioni.

Licha ya maafisa kukana , lakini vyombo vya habari vinadhani kuwa Musharaff alikuwa akilengwa.

Amenusurika majaribio mawili ya kutaka kumuua mwezi Desemba 2003.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com