1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Islamabad. Imran Khan afunguliwa mashtaka ya ugaidi.

15 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1F

Polisi wa Pakistan wamemfungulia mashtaka kiongozi wa upinzani Imran Khan chini ya sheria ya kupambana na ugaidi baada ya kuonekana tena hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kutangazwa hali ya hatari.

Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa lakini afisa mmoja amesema kuwa Khan amekuwa akichafua amani kwa kuhudhuria katika maandamano ya wanafunzi dhidi ya rais jenerali Pervez Musharraf. Mkuu wa polisi wa mji wa Islamabad amemshutumu Khan hapo kabla kwa kusambaza chuki pamoja na kuchochea watu kuipinga serikali. Khan ambaye ni mchezaji wa zamani wa mchezo wa kriket alikamatwa baada ya kwenda katika chuo kikuu cha Punjab mjini Lahore. Wakati huo huo waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto ameendelea kuwa kizuizini nyumbani kwake mjini Lahore kumzuwia kuongoza maandamano dhidi ya sheria ya hali ya hatari, baada ya hapo kabla kumtaka Musharraf kung’atuka.