1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakaribisha ripori ya Marekani

Siraj Kalyango4 Desemba 2007

China yataka mgogoro utanzuliwe kidiplomasia

https://p.dw.com/p/CWpU
Stephen Hadley, mshauri mkuu wa rais wa Marekani kuhusu masuala ya amani akiwahutubia waandishi habari kuhusu ripoti y makundi ya upeleleziPicha: AP

Iran imekaribisha ripoti ya Marekani iliotolewa kuhusu mpango wa Nuklia.

Ripoti inasema kuwa Iran iliacha mpango wake wa silaha za Nuklia miaka zaidi ya mitatu iliopita.

Matokeo ya ripoti hii yanakwenda kinyume na madai ya utawala wa Bush kuwa Iran ilikuwa inapanga kutengeneza Bomu la atomiki.

Utawala wa Tehran umesema kuwa sasa ni bayana kuwa serikali ya Kiislamu haina mipango ya kutengeneza silaha za nuklia bali mpango wa matumizi ya amani kama vile nishati.

Ripori ya pamoja ya vyombo vya upelelezi vya Marekani –NIE kwa kifupi, inasema kuwa Iran iliachana na mpango wa kutengeneza silaha za nuklia mwaka wa 2003.Iran, kwa upande wake, inasema haijawahi kuwa na mpango kama huo bali ule wa kuzalisha umeme.

Mshauri wa rais Bush kuhusu masuala ya usalama, Stephen Hadley, ameikaribisha ripoti hiyo akisema kuwa utabiri wao ulikuwa sawa…

'…kwa upande mwingine hii inahakiksha kuwa tulikuwa wa kweli kuhofia Iran kuwa ilikuwa inataka kutengeneza silaha za nuklia.Kwa upande mwingine inatuambia kuwa tumepiga hatu amoja mbele kujaribu kuhakikisha kuwa hilo halifanyiki.Hata hivyo pia inatuambia kuwa uwezekano wa Iran kupata silaha hizo baado ni tatizo kubwa.kamati ya upepelezi inaamini kuwa Iran iliachana na mpango wake wa silaha za nuklia mwaka wa 2003 na pia inaamini kuwa nchi hiyo ilikuwa haijauanzisha tena mpango huo hadi katikati ya mwaka wa huu wa 2007' ...

amesema Hadley.

Hata hivyo Israel, hasimu mkuu wa Iran inasema kuwa, huenda utawala wa Tehran,umesha anza tena mpango wake kuhusu silaha,licha ya kuusimamisha kwa mda.

Aidha ripoti hii, inaweza ikakwamisha juhudi za Marekani za kuzishawishi nchi zingine za kutaka Iran iwekewe vikwazo kupitia umoja wa Mataifa kwa kukaidi ombi la kuachana na urutubishaji wa madini ya Uranium.Urutubishaji huo sio tu unachangia matumizi yasio ya kijeshi na hata pia ya kijeshi.

Waziri wa mashauri wa kigeni wa Iran, Manouchehr Mottaki, akitoa maoni kupitia redio ya taifa kuhusu ripoti ya Marekani,amenukuliwa kusema kuwa anaikaribisha kwani nchi zilizokuwa na shaka kuhusu mpango wake kuwa wa amani sasa watabadili maoni yao.

Mvutano kati ya nchi hizo mbili uliongezeka kuwa mbaya miezi michache iliopita baada ya kauli ya rais Bush mwezi wa Oktoba kuwa Iran ikiwa na silaha za nuklia yaweza kusababisha vita vikuu vya tatu vya dunia.

Vikwazo vya aina mbili vya Umoja wa mataifa- dhidi ya Iran vimepitishwa bila kupingwa,lakini baada mvutano wa kidiplomasia miongoni mwa nchi tano ambazo ni za kudumu katika baraza la usalama la Umoja wamataifa.Nchi hizo ni Marekani, Urusi, China,Ufaransa,Uingereza na Ujerumani.

China kwa upande mwingine leo imehimiza kufanyika majadiliano ili kutanzua mgogoro wa kinuklia wa Iran.Mwito huo imeutoa siku moja tu baada ya ripoti ya vikosi vya upelelezi vya Marekani ambayo inapunguza hoja za kutaka Iran kuchukuliwa hatua kali.Msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya China amesema waziri wake Yang Jiechi, amezungumza kwa simu na cheo somo wake wa Marekani-Condoleeza Rice, baada ya kutolewa ripoti hiyo.

Msemaji huyo,ameendelea kuwa, waziri Yang, katika mazungumzo yake, amesisitizia umuhimu wa njia za kidplomasia kama njia muafaka ya kutanzua mgogoro akisema kuwa njia hiyo inasaidia malengo ya jamii ya kimataifa ikiwemo China na Marekani.

Ripori ya Marekani,inayojumulisha mashirika ya upelelezi ya Marekani 16, hata hivyo imesema haijaeleweka baado ikiwa Iran ilitaka silaha za nuklia na kuwa kusimamisha mpango wake kunamaanisha kuwa ni kazi ya shinikizo la dunia kinyume na ilivyofikiriwa.