1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yakanusha madai ya Marekani kuhusu kisa cha manuari zake na mataboti za Iran

9 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cn78

TEHRAN:

Jeshi la kimapinduzi la Iran limeilaumu Marekani kwa kubuni picha za video kuonyesha kuwa mataboti za Iran zikisumbua manuari za kijeshi za Marekani katika mlango wa bahari wa Hormuz.

Jumanne,jeshi la Marekani lilitoa mkanda wa Video ukionyesha mataboti za Iran zikikaribia manuari za Marekani na kuzitishia kuzilipua.Jeshi la kimapinduzi la Iran linasema, mkanda huo umebuniwa tu.Kituo cha televisheni cha kiarabu cha Iran-Al-Alam pia kimetoa tangazo la kukana likinukuu duru za jeshi la kimapinduzi.Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitoa video ya dakika nne ikionyesha kile maafisa wa Marekani walichokiita mvutano uliodumu dakika 20.