Iran na Umoja wa ulaya watakutana kama ilivyopangwa alkhamisi ijayo | Habari za Ulimwengu | DW | 27.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Iran na Umoja wa ulaya watakutana kama ilivyopangwa alkhamisi ijayo

Teheran:

Mkutano kati ya mkuu wa tume ya Iran katika mazungumzo ya kinuklea Ali Larijani na muakilishi mkuu wa siasa ya nje wa Umoja wa Ulaya,Javier Solana utafanyika kama ilivyopangwa May 31 ijayo.Habari hizo zimetangazwa hivi punde na wizara ya mambo ya nchi za nje ya Iran mjini Teheran.”Mazungumzo yatafanyika kama ilivyopangwa .”Taarifa ya wizara ya mambo ya nchi za nje imesema na kuongeza kwamba mahala halisi yatatangazwa baadae.Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje Mohammes Ali Hosseini alisema hapo awali kwamba mazungumzo hayo yaliyokua yafanyike alkhamisi ijayo nchini Hispania yameakhirishwa kwa ridhaa ya pande zote mbili.Mazungumzo hayo yamelengwa kusaka njia za kumaliza mvutano uliosababishwa na mradi wa Iran wa kurutubisha maadini ya kinuklea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com