1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

INSTANBUL : Mkutano wa usalama wa Iraq kuanza leo

3 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7AJ

Duru ya pili ya mazungumzo makubwa ya kimataifa juu ya kuimarisha usalama na utulivu nchini Iraq inatazamiwa kuanza katika mji wa Instanbul nchini Uturuki leo hii.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zote sita majirani wa Iraq wanakutana pamoja na wanadiplomasia waandamizi kutoka Umoja wa Mataifa,Kundi la Mataifa Manane lenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani na taasisi za kimataifa za Kiarabu na za Kiislam.Duru ya kwanza ilifanyika hapo mwezi wa Mei lakini licha ya kuwepo kwa nia njema matokeo yake yamekuwa haba.

Hata hivyo agenda ya mkutano huo imetawaliwa na mpango wa Uturuki kuingia kaskazini mwa Iraq kuwaandama waasi wa Kikurdi.

Katika siku za hivi karibuni Uturuki imewakusanya wanajeshi wake 100,000 mpakani kujiandaa kwa hatua hiyo.