1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IMF yazindua sera mpya ya rushwa kwa wanachama

Josephat Charo
23 Aprili 2018

Shirika la fedha la kimataifa IMF limezindua sera mpya inayolenga kupambana na rushwa na athari zake katika ukuaji wa uchumi katika nchi wanachama.

https://p.dw.com/p/2wWac

Sera hiyo mpya pia inalenga kulitafutia ufumbuzi tatizo kuhusu jinsi mataifa tajiri yaliyostawi kiuchumi duniani yanavyochangia kusababisha rushwa katika nchi zinazoendelea, kwa kushindwa kuzuia hongo na utakatishaji fedha au kuruhusu umiliki wa makampuni na watu wasiojulikana. Je, sera hii inatekelezeka? Na je shirika la IMF kweli lina uwezo wa kuyabana mataifa makubwa? Haya ni miongoni mwa maswali ambayo Josephat Chari alimuuliza Profesa wa uchumi Honnest Prosper Ngowi, jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Kwanza alitaka kujua mtazamo wake kuhusu sera hii mpya. Unaweza kusikiliza mahojiano hapo chini.