1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wasiokua na kazi nchini Ujerumani yazidi kupungua

Oummilkheir29 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUhd

Nürnberg:

Idadi ya wasiokua na kazi nchini Ujerumani ni ya chini kabisa kuwahi kushuhudiwa tangu miaka 15 iliyopita.Shirikisho la ajira mjini Nürnberg linasema watu milioni tatu na laki tatu na 78 elfu wameandikishwa hawana kazi.Idadi hiyo imepungua kwa watu 55 elfu ikilinganishwa na idadi kama hiyo ya wasiokua na ajira waliaondikishwea mwezi October uliopita-na watu laki sita na 20 elfu ikilinganishwa na mwaka mmoja uliopita.Mkuu wa shirikisho la ajuira Frank Jürgen Weise anasema matokeo ya kutia moyo katika soko la ajira yataendelea pia mwakani.