1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya Wamisri waliojitokeza kupiga kura ni ya juu kabisa

Mohammed Khelef3 Desemba 2011

Zaidi ya Wamisri milioni nane walipiga kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa kwanza huru baada ya miaka 60, ikiwa ni sawa na 62%, ambayo ni kubwa kabisa katika historia ya karibuni ya nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/13LxY
Mpigakura wa Misri akipita mbele ya mabango ya kampeni.
Mpigakura wa Misri akipita mbele ya mabango ya kampeni.Picha: dapd

Chama cha Udugu wa Kiislamu na hasimu wake, chama cha kihafidhina cha Salafi, vina uwezekano mkubwa wa kupata wingi wa kura. Lakini kuna wasiwasi wa athari za serikali yenye msimamo mkali wa Kiislamu kwa uhuru binafsi wa watu, na kwa uchumi wa Misri unaoongozwa na utalii. Uchaguzi wa wabunge unafanywa kwa awamu tatu tafauti, ambapo utakamilika mwezi Machi mwakani kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais katikati ya mwaka ujao. Baraza la Kijeshi, lililoingia madarakani baada ya Hosni Mubarak kutimuliwa, limeahidi kuwa hadi kufikia mwezi Julai mwakani litakuwa limeshakabidhi serikali kwa utawala wa kiraia.