1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliouwawa Gaza yafikia 59

15 Mei 2018

Maandamano makubwa yanatarajiwa tena leo hii,(15.05.2018) ikiwa ni baada ya jeshi la Israel kuwauwa Wapelestia 59 wakati wa vurugu na maandamano katika eneo la mpakani la Ukanda wa Gaza.

https://p.dw.com/p/2xjyA
Gaza Israel Konflikt  - Beerdigung
Ndugu wa Mahmoud Abu Teima ambae aliuwawa kwa makombora ya IsraelPicha: picture-alliance/AA/A. Amra

Mauwaji hayo ambayo yameingia katika rekodi ya kuwa mabaya zaidi kutokea kwa siku katika mgogoro huo kwa miaka kadhaa, yanatokana na hatua ya waandamanaji kupinga hatua ya Marekani kufungua ubalozi wake mjini Jerusaleem.

Wapalestina leo hii wanaadhimisha siku wanayoiita Nakba, yaani Janga, siku ambayo  zaidi ya watu 700,000 ambao walikimbia au kufukuzwa katika vita ya mwaka 1948 vilivyozingirwa na uanzishwaji wa taifa la Israel. Kumbukumbu hiyo inakuja siku moja baada ya Marekani kuuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv, kwenda katika jiji lenye mgogoro la Jerusalem , hatua mabayo imewakasirishwa Wapalestina na kulaaniwa na jumuiya ya kimataifa.

Mbinu za mauwaji ya Gaza

Gaza Israel Konflikt  - Beerdigung
Binti na mama wakiwa katika kilioPicha: picture alliance/Xinhua/K. Omar

Wizara ya Afya ya Gaza imesema idadi kubwa ya wakazi wa maeneo ya Gaza, ambao waliuwawa jana, vifo vyao vilitokana na wadunguaji. Idadi hiyo ya vifo inajumuisha mtoto mdogo ambae alipoteza maisha baada ya kuvuta gesi ya mabomu ya kutoa machaozi, akiwa miongoni mwa watoto wenghine wa chini ya umri wa miaka 16.

Takribani watu wengine 2,400 wamejeruhiwa katika siku hiyo ya umwagikaji damu zaidi katika mgogoro wa Israel na Palestina tangu vita vya Gaza vya mwaka 2014. Afisa mwandamizi wa kundi la Hamas Khalil al-Hayya ameapa kuwa maandamano ya Gaza yataendelea leo hii. Amesema kundi hilo halitavumilia  uhalifu unaofanywa katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la mjini Jerusalem

Katika hatua nyingine China imeitaka  Israel kujizuia na operesheni zake katika eneo la mpaka wake na Gaza baada ya mauwaji ya Wapalestina 59, waliuwawa wakati wa maandamano. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lu Kang amesema taifa lake linapinga vitendo vya vurugu ambavyo vinawalenga watu wasiokuwa na hatia. Na kuzitaka pande zote katika eneo hilo kuacha kuhasimiana.

Suluhisho la mzozo wa Mashariki ya Kati

Zaidi Lu Kang alisema "China wakati wote ina amini kwamba utatuzi wa suala la Jerusalem, unapaswa kufanyika kwa kuzingatia maazimio yaliopo ya Umoja wa Mataifa, kwa mazungumzo kati ya Palestina na Israel."

China imekuwa ikiipigia chapuo Israel kwa muda mrefu kutokana na mahusiano yao ya kiuchumi, kidiplomasia na kijeshi. Kwa upande mwengine Afrika kusini na Uturuki zimewaita myumbani mabalozi wao walioko Israel.

Kufuatia hali hiyo kwa upande wao Iran imesema maafisa wa Israel wanapaswa kushitakiwa kama waarifu wa kivita kutoka na mauwaji ya waandamanaji.  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bahram Ghasemi ameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya Israel. Aidha nae Spika wa Bunge la Iran Ali Larijani ameuzungumzia uamuzi wa Israel kuuhamisha ubalozi wake Jerusalem kuwa ni sehemu ya kuzidharau taasisi za kimataifa, ikiwa sawa kabisa na kujiondoa katika mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris na makubalianbo ya nyuklia ya Iran.

Urusi kwa upande wake imeyataka mataifa na hasa ambayo yanashiriki katika mchakato wa upatanishi wa mgogoro wa Mashariki ya Kati kujiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuchochea zaidi mvutano katika ukanda huo, katika kipindi hiki ambacho pia duru zinaonesha huko marioketi ya Israel yakiwasha taa za tahadhari kwa upande wa kusini mwa taifa hilo ulio karibu na mpaka wa Gaza.

Mwandishi: Sudi Mnette RTR/AFP/APE
Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman