1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ian Smith afariki dunia.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ69

Harare. Kiongozi wa zamani wa utawala wa wazungu wachache nchini Zimbabwe, Ian Smith amefariki nchini Afrika kusini akiwa na umri wa miaka 88.

Katika mwaka 1965 Smith aliongoza wazungu wenzake laki mbili na nusu nchini Rhodesia kutangaza uhuru bandia kutoka Uingereza kuliko kukubali pendekezo la utawala wa Waafrika waliowengi. Alibakia madarakani kama waziri mkuu hadi wapiganaji wa chini kwa chini walipomlazimisha kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano na suluhisho la amani katika mwaka 1979. Uchaguzi ulifanyika mwaka uliofuata, wakati Rhodesia ilipopata utawala wa Waafrika waliowengi na kubadilishwa jina kuwa Zimbabwe, na Robert Gabriel Mugabe kuwa waziri mkuu wake. Smith aliendelea kupinga utawala wa Mugabe, hata pale baada ya sheria ya viti maalum vilivyotengwa kwa ajili ya wazungu wachache kuondolewa mwaka 1987.