1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hukmu ya Mubarak magazetini

4 Juni 2012

Huu ya rais wa zamani wa Misri,Hosni Mubarak,mkutano mkuu wa chama cha mrengo wa shoto Die Linke ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

https://p.dw.com/p/157Za
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarakl akisikiliza hukmu dhidi yakePicha: dapd

.Tuanzie lakini Cairo ambako magazeti mengi ya humu nchini yanahisi kifungo cha maisha dhidi ya rais wa zamani hakisaidii kutuliza ghadhabu za wananchi.Gazeti la "Döbelner Anzeiger linaandika:"Wamisri wengi wanahisi hukmu hiyo si kali vya kutosha na wala hailingani na maovu yaliyotokea.Kwa maoni yao,hakuna shaka yoyote,rais huyo wa zamani amejitaja mwenyewe kuwa mwenye hatia.Wa Misri wengi wanashindwa kuikubali hukmu hiyo ,wanahisi si ya haki.Ghadhabu za umma zimechanganyika na hisia za kutokuwa na imani na mfumo wa sheria na hofu kwamba hukmu dhidi ya rais huyo wa zamani itamaanisha mwisho wa kutathminiwa kisheria enzi za Hosni Mubarak.Kunyamaza na kumezea haustahiki kuwa muongozo wa Misri mpya,sawa na chuki na miito ya kulipiza kisasi dhidi ya wafuasi wa mtawala huyo wa zamani wa kiimla.Yote mawili yatazidisha mtengano kati ya kambi mbili na kuzidi kuitumbukiza katika hali ya mtafaruku nchi hiyo.

Gazeti la "Heibronner Stimmer" linahofia madhara ya hukmu ya Mubarak kwa duru ya pili ya uchaguzi wa rais.Gazeti linaendelea kuandika:"Ushawishi wa utawala wa zamani umezuwia kujulikana ukweli kuhusiana na maovu yaliyofanywa na polisi na idara za upelelezi.Hata mahakimu katika kesi ya Mubarak wamelalamika hawakupata msaada wowote kutoka idara husika.Rushwa inazidi kutawala,na kwa upande wa kisiasa,mfarakano miongoni mwa wananchi ni mkubwa.Wanamapinduzi wamevunjika moyo kupita kiasi.Pindi waziri mkuu wa zamani Ahmed Shafiq,mwakilishi wa utawala wa zamani,akishinda uchaguzi wa rais,basi Misri itajikuta ikikumbwa na hatari ya kuzongwa na balaa la machafuko.

Die Linke Bundesparteitag Göttingen Bernd Riexinger und Katja Kipping
Uongozi shirika wa die Linke Bernd Riexinger (kushoto) na Katja KippingPicha: dapd

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamemulika pia mvutano uliopo katika chama cha mrengo wa Shoto-Die Linke,kati ya kundi la sehemu ya mashariki ya Ujerumani na lile linalotokea sehemu ya magharibi ya Ujerumani.Kuhusu mkutano mkuu wa Die Linke huko Göttingen,Gazeti la Volksstimme linaandika:"Sura halisi ya mfarakano kati ya wafuasi wa upande wa mashariki na wale wa upande wa magharibi imebainika kupitia ile hali Gregor Gysi na Oscar Lafontaine walivyokuwa wakitupiiana maneno wakati wa mkutano huo mkuu.Biografia ya wanaswiasa wa Die Linke kutoka mashariki inatofautiana sana na ile ya wenzao kutoka Magharibi .Ndio maana ni shida kuashiria mustakbal wa chama hicho kwa daraja ya taifa.

Gazeti la "Nordsee-Zeitung" linaandika:"Mpango wa Die Linke ambao ungeweza kutumika kwa Ujerumani nzima,umevurugika.Hakuna mkakati wa pamoja,hakuna uongozi wa pamoja hakuna vuguvugu la kijamii linaloweza kuangaliwa kama shina.Mivutano ,majivuno na pengo linalowatenganisha walio mashariki na wale wa magharibi.Hiyo ndio sura halisi.Viongozi 2 shirika walioteuliwa Göttinger ,Katja Kipping na Bernd Riexinger watazidi kulipanua pengo hilo badala ya kulipunguza kwasababu wote wawili,hakuna mwenye usemi.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman