1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hujuma za madage ya marekani zagharimu maisha ya wanawake na watopto 15 Iraq

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GK

Baghdad:

Jeshi la Marekani nchini Irak linasema limewauwa wanawake na watoto wasiopungua 15 katika hujuma za jeshi la wanaanga zilizogharimu maisha ya watuhumiwa 19 wa Al Qaida.Hilo ni shambulio baya kabisa dhidi ya raia wa kawaida kuwahi kushuhudiwa tangu Marekani ilipoivamia Iraq mnamo mwaka 2003.Hujuma hizo za jana zimetokea katika wakati ambapo Umoja wa mataifa umevitaka vikosi vya Marekani vichunguze visa vya mauwaji na kuchapisha hadharani matokeo ya uchunguzi wao.Wakati huo huo,katika mji wa Tuz,kaskazini mwa Iraq,mtu aliyeyatolea mhanga maisha yake,amesababisha kifo cha mtoto mmoja na kuwajeruhi watu wengine zaidi ya 20,alipojiripua katika uwanja wa michezo.