1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Holland yaitoa Slovakia kwa mabao 2:1

28 Juni 2010

Afrika nzima yaishangiria Ghana

https://p.dw.com/p/O5BX
Robin van Persie wa holand anyan'ganyia dimba.Picha: AP

Holland imeilaza na Slovakia mabao 2:1 na imeingia robo-finali ya Kombe hili.Bao la kwanza lilitiwa na Arjen Robben,anaeichezea bayern munich, tayari mnamo dakika ya 17 ya mchezo.Mnamo dakika ya 82 ya mchezo,Sneider akaipatia Holland bao la pili.Kipa wa Slovakia,aliokoa maridadi ajabu mabao kadhaa na ikionekana kana kwamba, Holland ingebidi kuridhika na bao lao la kipindi cha kwanza,Sneider akaipatia Holland bao la pili.Katika dakika za kufidia, Slovakia ilijiaptia bao la penalty la kufuta machozi na kuaga Kombe la dunia 2010. Wittek alietiwa munda na kipa wa Holland, ndie alitia bao la Slovakia.

Holland, imewahi kufika finali ya Kombe la dunia mara 2:kwanza 1974 iliponyimwa Kombe na Ujerumani na tena miaka 4 baadae huko Argentina,Kombe lililpokwenda kwa wenyeji. Mwaka huu, wanadai wadachi wakitamba na Arjen Robben ni mwaka wake. Slovakia,iliipiga kumbo Itali, mabingwa wa dunia ili kuiweka miadi ya leo na Holland.

Baada ya Ujerumani jana kuikon'goa meno Uingereza kwa mabao 4-1 na Argentina kuichapa Mexico mabao 3-1, Ujerumani imepanga miadi na Argentina katika marudio ya mpambano kama huo katika kombe lililopita la dunia 2006 Ujerumani. Ujerumani, ilitamba na baadae kupokonywa Kombe na Itali siku ya finali.

Wakati mashabiki wa dimba nchini Uingereza, wanaomboleza, wale wa Ujerumani, wanashangiria chipukizi wao akina Podolski, Mueller na Ozil kwa kuwalipizia kisasi Waingereza kwa pigo la Wembley, 1966, pale England ilipoipokonya Ujerumani Kombe la dunia.

Isitoshe, wajerumani ,wanadai wamelipiza jana kisasi kwa lile bao la kutatanisha la Uingereza-bao lao la 3 kabla Uingereza mwishoe, kuishinda Ujerumani kwa mabao 4:2 kufuatia kurefushwa mchezo hapo 1966.

Gazeti kubwa la Ujerumani BILD, liliandika kichwea hiki cha habari hii leo: "Boys, we love you"-watoto, tunawapenda. Hizo ni pongezi kwa jinsi chipuklizi wa Ujerumani, walivyo wazima akina Wayne Rooney, nahodha Steven Gerrad na Lempard.

Bao la Lampard, lililoingia kimiyani lakini, lilikataliwa, linalipiza kisasi cha bao la 1966. Wakati Waingereza hawakuungama hadi sasa miaka, 44 baadae, kuwa bao lile halikuwa bao, Wajerumani , wanaungama kwamba bao la jana lilivuka chaki na ni halali. Isipokuwa Rifu, amelikataa na wanafurahia hivyo.

Kwani, laiti bao lile lingekubaliwa na kufanya matokeo suluhu 2:2, haijulikani mchezo wa jana ungechukua mkondo gani na kumalizika vipi.

Hata kocha wa Uingereza, mtaliana Fabio Capello, akiipongeza Ujerumani kwa jinsi ilivyocheza; amedai bao lile lililokataliwa, ndilo liliichimbia kaburi Uingereza na kuizika.Capello:

"Nina hakika lile kosa kubwa alilofanya rifu, ndilo lililochangia kutolewa nje ya Kombe la Dunia."

Je, Waingereza watambakisha kocha Capello ? Binafsi, amesema angependa kuendelea kuwa kocha wa England.Lukas Podolski, alietia bao la pili lililofuatia lile la Miroslav Klose, alisema:

"Bila ya shaka, tunaujua uwezo wetu,lakini, sasa tusifanye uzembe tulioufanya baada ya kuishinda Australia.

Tunapaswa kuendelea kutia fora. Kumebakia mashindano 3 ambayo tunataka kuyakamilisha."

Alisema Lukas Podolski akiashiria hapo Ujerumani imepania kuilaza Jumamosi iliopita Argentina na kukata tiketi ya nusu-finali na baadae finali.Ushindi wa Ujerumani jana ulimvutia pia Kanzela Angela Merkel aliewapongeza chipukizi wake.Alisema,

"Ulikuwa mchezo wa kupendeza kabisa na ushindi mkuu. Nimefurahishwa mno; na inastahiki kuipongeza timu ya Ujerumani na kuwaambia endeleeni vivyo hivyo."

Ijumaa ijayo, Ghana na Uruguay, zitanyan'ganyia nafasi ya kucheza nusu-finali katika Soccer city Stadium.Ikiwa Ghana,itatamba siku hiyo, itavunja rekodi zilizowekwa na Simba wa nyika Kameroun, 1990 huko Itali na Senegal, 2002 huko Korea ya kusini na Japan-kupindukia robo-finali.

Ghana, iliwasili robo-finali ya timu 8 za mwisho, ilipoipiga kumbo juzi Marekani mabao 2:1 huko Rustenburg. Uruguay iliipiga kumbo Korea ya kusini pia kwa mabao 2:1 huko Port Elizabeth.

Afrika nzima iko nyuma ya Black Stars-Ghana na nyota yake ni tumaini la bara zima kama mwanamichezo wetu George Njongopa, alivyogundua mitaani huko Tanzania:

Mwandishi: Ramadhan Ali /AFPE

Uhariri:Miraji Othman