HELSINKI: Mkutano kuhusu Cyprus umeahirishwa | Habari za Ulimwengu | DW | 02.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HELSINKI: Mkutano kuhusu Cyprus umeahirishwa

Umoja wa Ulaya umeahirisha mkutano uliopangwa kufanywa siku ya Jumapili kujadili mgogoro wa Cyprus.Finland iliyoshika wadhifa wa rais wa baraza la umoja huo,imesema haikuwezekana kuwakusanya pamoja washirika wote wa mkutano huo.Inasemekana kuwa Uturuki haipo tayari kukaa katika mkutano mmoja pamoja na wajumbe wa Cyprus.Umoja wa Ulaya huenda ikazuia majadiliano yanayofanywa pamoja na Ankara kuhusika na ombi la Uturuki la kataka kujiunga na umoja huo,ikiwa Uturuki itaendelea kukataa kuitambua Cyprus iliyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com