1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILIGENDAMM:Raia wote wapigwa marufuku Heiligendamm

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvz

Mahakama moja hapa Ujerumani inazidi kuweka mbinyo kuzuia maandamano kufanyika Heiligendamm kutakakofanyika mkutano wa kilele wa kundi la mataifa nane yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni G8.Mahakama katika mji wa kaskazini mashariki wa Griefswald ilibadilisha uamuzi wa awali ulioruhusu maandamano kufanyika katika eneo lililo na umbali wa mita 200 kutoka uzio wa mkahawa kutakakofanyika mkutano huo wa kilele.Raia wote wamepigwa marufuku kufika kwenye eneo la Heiligendamm.

Kundi la wanaharakati linapanga kuandamana tarehe 7 mwezi huu ili kufikisha kesi hiyo katika mahakama kuu.Nchi ya Ujerumani inafanya juhudi zote zile ili kuhakikisha kuwa maandamano hayafanyiki wakati wa kikao hicho muhimu kama ilivyotokea awali hususan mjini Genoa nchini Italia mwaka 2001.