1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HEILIGENDAMM:Afrika kuongezewa misaada kikao chaingia mkondo wa mwisho

Mkutano wa mataifa yaliyostawi kiviwanda G8 unaingia mkondo wake wa mwisho hii leo mjini Heiligendamm hapa Ujerumani.

Viongozi wa kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda G8 wameahidi dola bilioni 45 kwa bara la Afrika kupambana na Ukimwi na magonjwa mengine yanayosababisha idadi kubwa ya vifo. Mpango huo umetangazwa rasmi na Bi Angela Merkel Kansela wa Ujerumani aliye pia muandalizi wa mkutano huo.

Kundi hilo aidha limetangaza tena ahadi ilizotoa miaka miwili iliyopita za kuongeza msaada kwa dola bilioni 37 zaidi kwa bara la Afrika ifikapo mwaka 2010.

Viongozi hao kwa upande mwingine wanatoa wito kwa serikali za mataifa ya Afrika kumaliza ufisadi na rushwa.

Hapo jana viongozi hao waliafikiana kupunguza viwango vya gesi za viwanda ili kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.Kikao hicho aidha kinatoa wito kwa Korea Kaskazini kuacha kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu vilevile kusitisha mpango wake wa nuklia.

Viongozi wa mataifa ya Ghana,Algeria,Nigeria na Senegal vilevile,Umoja wa Afrika vilevikle NEPAD waliwakilisha bara la Afrika kwenye kikao hicho.Viongozi wa G8 wanasema wako tayari kuwekea nchi ya Sudan vikwazo kwa kutokubali kupelekwa kwa kikosi kilichoimarishwa cha Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa katika eneo la ghasia la Darfur.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com