1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILIGENDAMM: Mkutano wa viongozi wa madola tajiri G-8 wakosolewa

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtG

Wanaharakati wanaotetea mazingira na wanaofanya kampeni ya kupiga vita umasikini duniani, wameulani mkutano wa kilele wa mataifa manane tajiri G-8 uliomalizika siku ya Ijumaa katika mji wa Heiligendamm,kaskazini mwa Ujerumani. Wanaharakati hao wamesema,makubaliano ya viongozi hao kuhusu Afrika na mabadiliko ya hali ya hewa si cho chote isipokuwa ni maazimio yasio na uzito wa kuhakikisha kuwa yanatekelezwa.Wakati huo huo mawakili wa wapinzani wa mkutano huo wa G-8 wametoa mashtaka rasmi dhidi ya polisi wakiwatuhumu kuwa waliwazuia baadhi ya waandamanaji katika hali zisizozofaa kwa binadamu,katika seli za wafungwa sawa na mazizi ya wanyama.Lakini kwa mujibu wa idara ya polisi, vipimo vya seli hizo za mpito viliambatana na viwango vya kisheria.Polisi imesema,watu 932 walikamatwa wakati na kabla ya mkutano wa kilele wa G-8,baada ya kundi la wafanya fujo kusababisha ghasia Jumamosi iliyopita,mjini Rostock kwenye maandamano yaliotangulia mkutano wa kilele.