1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HEILIGENDAMM: Kansela Merkel ameridhika na mkutano wa G-8

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtL

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesifu matokeo ya mkutano wa kilele wa mataifa manane tajiri yalioendelea kiviwanda G8 uliofanywa mji wa Heiligendamm,kaskazini mwa Ujerumani.Merkel alieleza kuwa maafikiano mbali mbali yamepatikana katika mada zilizo muhimu.Akasisitiza kuwa makubaliano yaliopatikana katika masuala muhimu, yanahusika na ulinzi wa mazingira na misaada kwa bara la Afrika.Siku ya Ijumaa, viongozi wa G8 waliahidi kutoa msaada wa Euro bilioni 44 kupambana na UKIMWI,homa ya malaria na kifua kikuu barani Afrika na vile vile kutekeleza ahadi zilizotolewa hapo awali kuongeza misaada ya maendeleo.Waziri Mkuu wa Uingereza,Tony Blair pia amesema,anaamini kuwa makubaliano yaliopatikana kwenye mkutano wa Heiligendamm,huenda yakasaidia kuweka lengo la kimataifa,kupunguza uzalishaji wa gesi ya kaboni dayoksaidi kwa asilimia 50,ifikapo mwaka 2050.