1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HEILEGENDAMM: Mkutano wa G8 wazinduliwa rasmi.

Wakuu wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, walikutana kwa dhifa rasmi ya chakula cha jioni kuzindua mkutano wao wa mwaka huu, mkutano ambao umegubikwa na tofauti za jinsi ya kukabiliana na hali ya hewa inayobadilika.

Viongozi wa mataifa hayo mapema jana walishauriana na mwenyeji wao, Kansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel, kabla ya kujumuika jioni kwenye mji wa kitalii wa Heilegendamm.

Vikao rasmi vinatarajiwa kuanza leo.

Tayari Rais George W. Bush wa Marekani ametangaza ataunga mkono juhudi za Bibi Merkel za kupunguza gesi zinazotoka viwandani lakini amekataa kutenga muda maalumu wa kutekeleza hayo.

Rais George Bush amesema anawania kuwa na mwafaka mpya utakaochukua mahala pa mwafaka wa Kyoto kuhusu mazingira.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com