1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAVANA: Castro ahutubia taifa

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCeg

Rais wa Cuba, Fidel Castro, ametoa ujumbe wake kwa taifa kupitia runinga kuadhimisha miaka 48 ya mapinduzi.

Katika hotuba yake iliyosomwa na mtangazaji wa televisheni, Fidel Castro amekiri kwamba anakabiliwa na wakati mgumu wa mapumziko baada ya kufanyiwa upasuaji kwenye utumbo wake mnamo mwezi Julai mwaka huu.

Ujumbe wa mwisho wa mwaka wa rais Castro ni wa kwanza tangu tarehe 28 mwezi Oktoba mwaka huu, alipoonekana katika ukanda wa video kumaliza uvumi wa kifo chake.