1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Havana. Afya ya kiongozi wa Cuba inatia shaka.

1 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCnm

Kiongozi wa Cuba Fidel Castro ameshindwa kujitokeza katika sherehe za kijeshi mjini Santiago, na kuleta hali ya kujiuliza kwa wengi juu ya afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80.

Maelfu walijikusanya katika mji wa mashariki wa Santiago kwa ajili ya gwaride la kijeshi ambalo ni maadhimisho ya mwaka wa 50 wa kuundwa kwa majeshi ya kimapinduzi ya Cuba.

Castro hajaonekana hadharani tangu alipofanyiwa upasuaji wa dharura na kumlazimisha kukabidhi madaraka kwa muda kwa mdogo wake Raul mwishoni mwa mwezi wa Julai.