1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatimaye Berlusconi ajiuzulu

13 Novemba 2011

Ofisi ya Rais Giorgio Napolitano imesema Rais amekubali kujiuzulu huko kwa Waziri Mkuu Silvio Berlusconi baada ya kukutana naye kwenye ikulu yake mjini Rome.

https://p.dw.com/p/139n4
Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi
Waziri Mkuu wa Italia, Silvio BerlusconiPicha: dapd

Berlusconi, mwenye umri wa miaka 75, alikuwa ameahidi kujiuzulu mara baada ya bunge kupitisha mpango wa kubana matumizi uliotakiwa na Umoja wa Ulaya. Bunge liliupitisha mpango huo kwa kura nyingi jana (12.11.2011) jioni, huku baraza la Senate likiwa limeshafanya hivyo tangu juzi.

Nafasi ya Berlusconi madarakani ilianza kuingia mashakani tangu Jumanne iliyopita, pale aliposhindwa kupata kura za kutosha bungeni. Mara tu habari za kujiuzulu kwa Berlusconi ziliposambaa, maelfu ya watu walikusanyika katikati ya mji mkuu, Rome, kushangiria kuondoka kwake. Nafasi yake inatazamiwa kuchukuliwa na kamishna wa zamani wa Umoja wa Ulaya, Mario Monti.

Mwandishi: Mohammed Khelef/ZPR
Mhariri: Sekione Kitojo