1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barrow asema ni mwamko mpya Gambia

5 Desemba 2016

Rais Mteule wa Gambia Adama Barrow amempongeza Rais anayemaliza muda wake Yahya Jammeh kwa kukubali kushindwa kufuatia uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita ambapo upinzani uliibuka na ushindi.

https://p.dw.com/p/2TlBy
Gambia neuer Präsident Adama Barrow
Picha: Getty Images/AFP/M. Longari

Akihojiwa na kituo cha utangazaji cha DW  Barrow amesema hatua ya Rais Jammeh kukubali kushindwa hasa baada ya kuwa madarakani kwa kipindi cha miaka 22 si jambo la kushangaza  kwani wananchi wa taifa hilo wamefanya uamuzi kupitia sanduku la kura na kuwa madaraka siku zote yanatolewa na wananchi kupitia uchaguzi.

Amesema hatua ya kwanza atakayofanya baada ya kuchukua rasmi madaraka mwezi Januari mwakani ni kuunda baraza la mawaziri litakalokuwa na watu makini na kuongeza kuwa kwa sasa kila jambo ni muhimu nchini Gambia  na hivo atalazimika kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo mzima wa serikali ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuleta mageuzi katika uchumi, kuboresha miundo mbinu na utendaji  wa mahakama pamoja na masuala yahusuyo vyombo vya habari. 

Rais anaemaliza mhula wake Yahya Jammeh
Rais anaemaliza mhula wake Yahya JammehPicha: Getty Image/AFP/M. Longar

Tume ya ukweli na suluhu itaundwa Gambia

Alipoulizwa iwapo atachukua hatua dhidi ya Rais wa sasa, Yahya Jammeh ambaye anatuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kuendelea kubakia gerezani hadi sasa baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzani, Rais huyo mteule wa Gambia alisema:  "walishindana katika uchaguzi kwa misingi wa kuleta mabadiliko na mabadiliko yamekuja . "Hatuna jambo lolote la kibinafisi dhidi ya mtu yeyote, lakini wakati tutakapoanza kazi rasmi tutafanya uchunguzi wa masuala mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanyika na uamuzi wetu utatokana na ripoti tutakayokuwa tumeipata kutokna na uchunguzi huo."Amewataka watu waondowe hofu akisisitiza watatenda haki kwa kila mtu kuambatana na sheria  "

Kuhusiana na hoja ya kuundwa kwa tume ya ukweli na maridhiano, Rais Jammehe alisema  hilo ni suala ambalo yeye na serikali yake wanatarajia lifanyike nchini humo akitolea mfano tume ya aina hiyo iliyoundwa baada ya utawala wa kibaguzi nchini Afrika Kusini.

Wagambia washangiria ushindi wa Adama Barrow
Wagambia washangiria ushindi wa Adama BarrowPicha: Reuters/T. Gouegnon

Viongozi wepya waajiandaa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa Gambia

Aidha kwa upande mwingine Adama Barrow alisema tayari yeye na viongozi wenzake wameanza kuchukua hatua kuhusiana na suala la kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa na kuwa ni jambo ambalo anataraji litafanyiwa kazi na serikali yake mapema iwezekanavyo kwa kufuata yale yatakayojiri kutokana na  tume ya ukweli na maridhiano itakayoundwa.

Akiuzungumzia juu ya uamuzi wa Rais Jammeh ya kuliondoa taifa hilo katika Jumuiya ya Commonwealth, kujiondoa pia katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu pamoja na hatua ya kulitangaza taifa hilo kuwa la kiisilamu Adama Barrow alisema: Uamuzi huu utabadilika na watarejea katika jumuiya ya Common wealth pamoja na kuendelea kuwa wanachama wa jumuiya mbalimbali za kimataifa. "Gambia inahitaji jumuiya za kimataifa, na ni nchi ndogo hatuwezi kujitenga, hakuna haja ya sisi kujiondoa kaatika mahakama ya ICC kwani mahakama hiiyo inafanya kazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa nchi zinafuata misingi ya utawala bora hivyo hatuwezi kabisa kujiondoa katika mahakama ya ICC"

Akizungumzia juu ya Rais Jammeh kutangaza taifa hilo kuwa jamhuri ya kiisilamu , Rais mteule Adama Barrow alisema taifa hilo haliwezi kuwa Jamhuri ya kiisilamu kwani lina watu wenye imani tofauti za kidini na kila mtu ana haki ya kufuata dini anayotaka na kuwa wanataka taiafa hilo liendelee na amani hivyo suala la jamhuri ya kiisilamu halipo tena.

 

Mwandishi: Isaac Gamba /DW

Mhariri      :Yusuf Saumu