1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE:Mugabe ainyooshea kidole Uingereza kwa hujuma inazomfanyia

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfb

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema kuwa Uingereza na nchi washirika wake wa Magharibi zimezidisha juhudi zao za kumuondoa madarakani kwa kufadhili vurugu katika nchi hiyo inayokabiliwa na hali mbaya ya uchumi.

Rais Mugabe ambaye amekuwa madarakani toka uhuru wa nchi hiyo mwaka 1980 alisema hayo jana wakati alipohutubia bunge la nchi hiyo.

Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 83 alitoa wito kwa nchi rafiki barani afrika na nje ya bara hilo kupinga hatua za kuupeleka mzozo wa Zimbabwe katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.