Harare. Mwingine apigwa na kujeruhiwa. | Habari za Ulimwengu | DW | 19.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Harare. Mwingine apigwa na kujeruhiwa.

Mwanachama mwingine wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change amejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa. Mwanachama huyo ambaye ni mbunge , Nelson Chamisa amesema kuwa alishambuliwa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare, ambako alikuwa anapanga kusafiri kwenda katika mkutano nchini Ubelgiji.

Anapatiwa matibabu hospitalini baada ya kupata mpasuko kichwani.

Serikali imekana kuwa majeshi yake yanahusika katika shambulio hilo. Hii inakuja wiki moja baada ya wajumbe kadha wa chama cha MDC kujeruhiwa vibaya na mtu mmoja aliuwawa baada ya polisi kuvunja mkutano wa sala ya maombi mjini Harare.

Kiongozi wa MDC Morgan Tsvangirai ni miongoni mwa wale waliopata matibabu hospitalini baada ya kupigwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com