1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Mugabe ataka kuwania urais mwaka ujao

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCE5

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe leo amekitaka chama chake cha ZANU – PF kiungane huku akitafuta kuungwa mkono agombee urais katika uchaguzi wa mwaka ujao nchini humo.

Wakosoaji wanasema rais Mugabe ameitumbukiza Zimbabwe katika mzozo mkubwa kupitia sera zake ikiwa ni pamoja na kuyateka mashamba ya wazungu na kuyapa Wazimbabwe.

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change, MDC, kimetangaza leo kwamba kiko tayari kukutana na chama tawala cha rais Robert Mugabe, ZANU-PF, lakini kikasema hakitarajii mazungumzo hayo kumaliza mzozo wa kisiasa na kiuchumi nchini Zimbabwe.

Jana viongozi wa kamati ya maendeleo ya mataifa ya eneo la kusini mwa Afrika, SADC, walimteua rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini aongoze juhudi za kuleta maridhiano baina ya vyama vinavyohasimiana nchini Zimbabwe.