1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HARARE: Akofu Ncube ajiuzulu

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQf

Askofu mkuu nchini Zimbabwe, Pius Ncube, amejiuzulu baada ya kukabiliwa na kashfa ya mapenzi.

Ncube ametajwa katika kesi ya uzinifu iliyowalishwa na mfanyakazi wa reli aliyedai kwamba mke wake, mhanzili katika ofisi ya askofu Ncube, alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na askofu huyo.

Runinga ya kitaifa nchini Zimbabwe imeonyesha picha zilizochukuliwa kisiri kutumia kamera zilizofichwa katika chumba cha kulala cha askofu Ncube ambazo zinamuonyesha askofu huyo akiwa pamoja na mwandishi huyo mnamo mwezi Julai mwaka huu.

Wakili wa askofu Ncube amekueleza kuonyesha picha hizo katika runinga kuwa juhudi ya serikali kumuaibisha mteja wake, ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa mkosoaji mkubwa wa rais Robert Mugabe.