1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANOI:60 wauwawa kwenye ajali ya kuporomoka daraja

26 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMR

Kiasi cha watu 60 wameuwawa na wengine wengi wamejeruhiwa au kutoweka baada ya daraja walilokuwa wakilijenga huko kusini mwa Vietnam Kuanguka.

Hata hivyo idadi kamili ya watu waliokuwa wakifanya kazi ya ujenzi kwenye eneo hilo hii leo haijulikanai.Waokoaji wanaendelea kuchimba vifusi kwenye eneo hilo kuwatafuta manusura.Kwa mujibu wa taarifa za polisi nchini humo kulitokea kama mripuko na kisha daraja hilo likaporomoka.Ajali hiyo inasemekana kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea katika nchi hiyo.Ujenzi wa daraja hilo ni mradi unafadhiliwa na Japan na ulitarajiwa kukamilika mwaka ujao.