1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hanoi. Watu milioni tano waathirika na kimbunga China.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HW

Zaidi ya watu milioni tano nchini China wameathirika na hali ya baada ya kimbunga Krosa, ambacho kililikumba eneo la pwani la kusini mashariki mwishoni mwa juma.

Kimbunga Krosa kilipungua na kuwa kimbunga cha kawaida cha maeneo ya tropiki lakini kimesababisha kukatika kwa umeme na kuathiri huduma za usafiri katika jimbo la mashariki la Zhejiang.

Katika maeneo mengine, idadi ya watu waliouwawa nchini Vietnam imepanda hadi zaidi ya watu 60 baada ya mafuriko mabaya sana kuwahi kutokea katika muda wa miongo kadha.

Nyumba za mamia kwa maelfu ya watu bado ziko katika maji na uharibifu unakadiriwa kufikia dola milioni 40.