HANOI: Rais Köhler akamilisha ziara ya Vietnam | Habari za Ulimwengu | DW | 22.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HANOI: Rais Köhler akamilisha ziara ya Vietnam

Rais wa Ujerumani Horst Köhler amekamilisha ziara yake nchini Vietnam,kwa kutoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwastahmilia zaidi wapinzani. Alisema,Ulaya ina wasiwasi kuhusika na matokeo ya hivi karibuni nchini Vietnam,baada ya mawakili wanaounga mkono udemokrasia kutiwa mbaroni.Baada ya mmkutano wake pamoja na Rais Nguyen Minh Triet,Köhler alisisitiza uhusiano wa nchi hizo mbili katika sekta za biashara na elimu. Kibiashara,Ujerumani ni mshirika mkubwa kabisa wa Vietnam barani Ulaya.Ziara ya Köhler barani Asia sasa inampeleka China.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com