1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG:Mmorocco akata rufaa kupinga hukumu

10 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCc4

Raia wa Morocco aliyehukumiwa hapo jana kifungo cha miaka 15 na mahakama ya Hamburg kwa kosa la ugaidi, amekata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Mounir el Motassadeq, alikutwa na hatia ya kuhusika na mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani Septemba 11 mwaka 2001.

Msemaji wa mahakama ya Hamburg amesema kuwa mawakili wa Motassadeq wamewasilisha rufaa kupinga hukumu hiyo.