HAMBURG:Mkutano mkuu wa chama cha SPD umeanza | Habari za Ulimwengu | DW | 26.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HAMBURG:Mkutano mkuu wa chama cha SPD umeanza

Mkutano mkuu wa siku tatu wa chama cha Social Demokratik unaanza hii leo mjini Humburg.

Wajumbe 525 wanatazamiwa kuuchagua uongozi mpya wa chama hicho pamoja na kuidhinisha mpango wa malipo ya muda mrefu ya watu wazima wasiokuwa na ajira.

Mpango huo unatazamiwa kuamua juu ya hatima ya ugomvi wa wiki kadhaa kati ya mwenyekiti wa chama cha SPD Kurt Beck na naibu kansela wa Ujerumani Franz Müntefering.

Inaaminiwa wengi wa wawakilishi wa SPD katika mkutano huo mkuu wanaunga mkono msimamo wa mwenyekiti wao Kurt Beck.

Nae kansela wa zamani Gerhard Schröeder amewatolea mwito wana SPD washikamane.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com