1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg yaongoza bado bundesliga

20 Oktoba 2008

Ligi mashuhuri za Ulaya zimerudi uwanjani kwa kishindo:

https://p.dw.com/p/FddD
Piotr Trochowski (hamburg)ashangiria bao lake.Picha: AP

Hamburg SV imebakia kileleni mwa Bundesliga licha ya kumudu suluhu tu ya bao 1:1 na Schalke.

Katika La Liga ,Valencia imeparamia tena kileleni mwa Ligi ya spain baada ya kuihilikisha Numancia inayoburura mkia kwa mabao 4-0.Huko Itali ,mabingwa Inter Milan walitunisha misuli jana na kunyakua usukani wa Serie A.

Bundesliga: Hamburg ilirudi kileleni mwa Ligi ya Ujerumani jana jioni ingawa ilimudu suluhu tu ya bao 1:1 na mahasimu wao Schalke.Mshambulizi alieiachamkono timu ya Taifa ya Ujerumani Kevin Kuranyi,aliongoza hujuma za Schalke lakini bila kufua dafu na baadae alibadilishwa na kuitwa uwanjani mahala pake kwa mzaliwa wa ghana Gerald Asamoah.

Hamburg ilikua ishike usukani tayari mnamo dakika ya 64 ya mchezo pale Ivica Olic alipoelekeza mpira langoni mwa Schalke lakini Petric mwakju wake uligonga mwamba wa lango la Schalke.

Baadae makocha wa timu hizo mbili wote kutoka Holland walizungumzia jinsi mchezo ulivyokwenda:Kocha wa Schalke aliueleza mchezo wa timu yake hivi:

"Kipindi cha kwanza Hamburg ilitamba zaidi ,lakini kipindi cha pili kilikua cha schalke ,kwani tiliongeza kasi na tulicheza kwa aina ambayo ilitubidi kucheza. "

Kocha wa Hambung Martin Joel, alisema:

"Tumeparamia kileleni mwa Bundesliga na hili ni jambo la kufurahisha.kipindi cha pili tuliregeza kidogo kamba na hapo Schalke wakacheza kidogo bora zaidi."

Kabla Hamburg kuparamia kileleni mwa Bundesliga jana jumapili, ilikua timu iliopanda msimu huu tu daraja ya pili ya Hoffenheim, iliokuwa kileleni alao kwa masaa 24.Hoffenheim ilitoka nyuma na kuizaba Hannover mabao 5-2.sasa inasimama nafasi ya pili baada ya hamburg kuunyakua jana usukani huo wa Ligi.Kocha wa Hoffenheim Reinicke alisema:

"Imevutia sana jinsi vijana wangu walivyojaribu kudhibiti mchezo tena na mwishoe, ilionekana kuwa kila hujuma waliofanyanya iliongoza nafasi ya kuweza kutia goli.Kwahivyo, tumeridhika mno na mchezo."

FC Colonge kama Offenheim ,ni timu nyengine iliopanda daraja ya kwanza kutoka ya pili msimu huu.Nayo pia inaendelea kutamba baada ya jana kushinda mpambano wake 3 mfululizo.Cologne iliizaba Energie Cottbus bao 1:0 na hivyo imeangukia nafasi ya 8 hata mbele ya mabingwa Bayern Munich ambao baada ya kutolewa jasho na Karlsruhe hadi dakika za mwisho, ilimudu ushindi nyumbani wa bao 1:0.

Akiueleza mwishoe, ushindi wa timu yake, kocha mashuhuri Christoh Daum alisema:

"Washambulizi wa Cottbus walidhibitiwa barabara,kwahivyo walinzi wa Cologne walikua imara kabisa.Upande wa washambulizi wetu umepoteza nafasi nyingi wazi za kutia mabao."Bayer Leverkusen ambayo ina miadi ijumaa hii ijayo na FC cologne kwa mpambano wa timu 2 za mtaani ,iliichapa Eintracht Frankfurt mabao 2-0.

Klabu ya 3 iliopanda msimu wa kwanza msimu huu kama Hoffenheim na Cologne ni Borussia Monchengladbach.Kinyume na wenzao hao 2, Monchengladbach imekua ikiburura mkia wa Ligi na ingawa ijumaa ilimudu suluhu ya mabao 2:2 na Bochum, ilitangaza jana kuwa na kocha mpya ambae kwa kweli ni kocha wake wa zamani Hans Meyer.B.Monchengladbach ilimtimua mapema mwezi huu kocha wake aliewapandisha daraja ya kwanza Jos Luhukay baada ya kushinda mpambano 1 kati ya 6 tangu kuanza msimu huu.

Katika Serie A-ligi ya Itali, mabingwa Inter Milan waliviringa ngumi jana na kuwatandika Roma mabao 4-0.Inter sasa ina jumla ya pointi 16-pointi 2 zaidi kuliko Udinese,Catania na napoli na płointi 3 kuliko AC Milan,Lazio,Fiorentina na Atalanta.AS Roma ingali inapepesuka ikiwa na pointi 7 kufuatia pigo lao la 4 na hii licha ya kurudi kwa nahodha wao Francesco Toti.

Valencia imeparamia tena kileleni mwa Ligi ya Spain baada ya jana kuiteketeza Numancia kwa mabao 4:0.Kama kawaida yao Valencia, shujaa wao jana alikuwa tena David Villa ambae hadi sasa ameshatia mabao 8.

Valencia iko pointi 2 mbele ya Sevilla na Villareal ziliopo nafasi ya pili kwa pointi zao 17 kwa 19 za valencia.

Nafasi ya 4 kwa pamoja ziko FC Barcelona na Real Madrid zikiwa na pointi 16 kila moja. Barcelona ilishinda kwa bao 1-0 dhidi ya Atletico Bilbao.lilikua bao la mkamerun Samuel Eto-o.

Katika champions League-kombe la klabu bingwa ambalo nusu-finali zake zilichezwa mwishoni mwa wiki, orodha ya watiaji mabao mengi inaongozwa na Stephen Worgu wa Enyimba iliocheza na Al Ahly ya Misri mwishoni mwa wiki.

Worgu ametia jumla ya mabao 13 kwa 7 ya Daouda Kamilou wa Contonsport Garoua ya Kameroun iliocheza na Dynamo ya Zimbabwe mwishoni mwa juma.Nafasi ya 3 ya watiaji magoli mengi katika kombe la klabu bingwa ni Ezenwa Otorogu wa Enyimba.Nafasi ya 4