1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamburg: Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani atahadharisha juu ya mpango wa kuishambulia kijeshi Iran.

28 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7C0

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, ameonya juu ya uwezekano wowote wa kuchukuliwa hatua za kijeshi dhidi ya Iran kutokana na mzozo juu ya harakati za kinyukliya za nchi hiyo. Waziri Steinmeier alisema hayo katika hotuba alioitoa mbele ya mkutano mkuu wa chama chake cha Social Democratic mjini Hamburg. Tamko hilo limekuja huku wasiwasi unazidi juu ya nia ya Marekani kuelekea Iran. Alisema kila kitu kifanyike kuzuwia kuweko silaha za kinyukliya katika Mashariki ya Kati, lakini alisisitiza kwamba Ujerumani lazima iendelee kujitahidi kutafuta suluhisho la kidiplomasia pamoja na Marekani, Russia na Uchina.

Katika mkutano mkuu huo chama cha SPD, leo kutapitishwa programu mpya ya kimsingi, ambapo chama hicho kinataka kuweko dola inayozingatia mahitaji ya kijamii. Jana wajumbe wa mkutano huo, kwa mshangao, walikubali kwamba kasi ya kuendesha magari katika barabara kuu iwe kilomita 130 kwa saa.