Hamburg , Ujerumani. Polisi wagundua miale katika maeneo mawili mjini Hamburg. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Hamburg , Ujerumani. Polisi wagundua miale katika maeneo mawili mjini Hamburg.

Nancy Pelosi na Bashar al Assad

Nancy Pelosi na Bashar al Assad

Polisi wa Ujerumani wamesema kuwa wamegundua ishara katika maeneo mawili nje na ndani ya mji wa Hamburg yanayohusishwa na jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko , ambaye amefariki mwezi uliopita kutoka na sumu la miale.

Usiku , polisi waligundua kiasi fulani cha miale katika nyumba moja ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara wa Urusi Dmitry Kovtun, ambaye alikutana na Litvinenko mjini London kabla ya kufariki.

Siku ya Jumamosi, polisi wamesema wamegundua kiasi kingine cha miale katika nyumba nyingine nje kidogo ya mji huo wa bandari. Kovtun , mmoja kati ya raia wawili wa Urusi ambao walikutana na Litvinenko katika hoteli ya Millennium mjini London Novemba mosi, anasemekana kuwa anapatiwa matibabu mjini Moscow kutokana na miale hiyo ya sumu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com