1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas yatishia kuzusha wimbi jipya la Intifadha

Oummilkheir16 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CcHI

Gaza:

Chama cha wapalastina wanaofuata itikadi kali – Hamas,kikiadhimisha miaka 20 tangu kilipoundwa,kimetishia kuanzisha wimbi jipya la Intifadha.Mapambano dhidi ya Israel yataeandelezwa,amesema kiongozi wa Hamas,Ismael Hanniyeh mbele ya umati wa wafuasi wake huko Gaza.Malaki ya wapalastina wa Gaza wamehudhuria mhadhara huo.Wanamgambo wa wa Hamas waliobeba silaha na kuficha nyuso zao walikua wakipiga doria.Kwa mujibu wa wafuasi wa Hamas, mhadhara kama huo uliokua uitishwe katika maeneo ya ukingo wa magharibi umezuwiliwa na rais wa autawalla wa ndani wa Palastina Mahmoud Abbas.